Ule uhasimu uliokuwepo kwa takribani miaka miwili sasa kati ya mastaa wakubwa na warembo Swahiliwood Jackline Wolper na Irene Uwoya hatimaye umefikia tamati baada ya kupatanishwa juzi. Wawili hao walidaiwa kuingia katika beef zito baada ya Uwoya kumsema Wolper vibaya kwenye media ambapo pia aliwahi kukaririwa na gazeti moja akiwa jijini Arusha akisema kuwa Wolper amemroga ili amshushe kwenye sanaa na yeye(Wolper) kuwa juu kisanaa kitu ambacho kilidaiwa kumuudhi sana Wolper. Hata hivyo habari nyingine zilizoifikia Xdeejayz mapema leo zinasema kuwa kumbe ugomvi huo chanzo ilikuwa ni kumgombea pedeshee mmoja mwenye pesa chafu.