Tanzania ni nchi ambayo mfumo wake wa kiuchumi na kisiasa ,unawafanya watu wengi kuwa na mkanganyiko .Hii ni kutokana na kutokuwepo kwa viashiria vya moja kwa moja kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa au kibepari.
Utata huo umewafanya wasomi na wanafalsafa mashuhuri nchini kuwa na mawazo tofauti.Hali hiyo imepelekea hata vijana katika shule kushindwa kujua ukweli yakinifu kuwa Tanzania ipo katika mfumo gani wa kiuchumi na kisiasa.Tutatumia fursa hii kuonesha mifumo yote miwli ili kuondoa utata unaozidi kuteka nyoyo za wasomi,wananaharakati na wachambuzi wa masuala ya kisiasa .suala hili limeleta utata hata katika katiba ya jamhuri ya muunganoi wa Tanzania ambapo baadhi ya watanzania wamejaribu kutoa maoni yao kuwa neno ujamaa lisijitokeze tena katika katiba mpya kwa kigezo kuwa hatuko katika ujamaa tena.Tupo katika mfumo wa kibepari.Miongoni mwa vifungu vinavyotaja ujamaa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ibara 3(1) “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na y a kijamaa, isiyokuwa na dini ,yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”
Suala hili limeleta utata wa hali ya juu kutokana na hoja kuwa Ujamaa haupo.Kupitia safu hii tunaona ni bora kujadili mifumo hiyo ili kuondoa utata kitaaluma.Kwa mujibu wa kitabu cha Mwl Nyerere (essay on socialism) (pg 1) anaelezea ujamma kwa kusema “Ujamaa ni mtazamo wa kifikra .Katika mtazamo huo wa wajamaa ni kuwa mfumo wa kisiasa upo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vyema katika Nyanja zote za kijamii” lakini wataalam wengine wazamivu katika taaluma ya falsafa za kijamaa kama Carl Marx yeye ana sema “Katika kitabu chake cha Communist Manifestal “Ujamma ni mfumo wa kiuchumi , kisiasa na kijamii wenye lengo la kutatua matatizo ya wafanyakazi na kuondoa unyonyaji uliokithiri “
Kwa mujibu wa mitazamo hiyo tunaweza kuona kuwa Ujamaa ni mfumo wa maisha uliojengwa ili kukidhi mahitaji ya msingi ya wananchi.Na mfumo huo umejikita kisiasa zaidi katika kuhakikisha iinatatua matatizo yote sugu ya kiuchumi na kisiasa.
Mfumo huo wa kijamaa ulianzishwa mara baada ya kutokea kwa athari ya mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution) (1750s) Mara baada ya mapinduzi ya viwanda (1750s) katika nchi ya Uingereza , baadae Ujerumani,Ufaransa na Marekani yalijitokeza matatizo ya msingi yaliyowakabili wafanyakazi wa viwandani katika nchi hizo za Ulaya na Amerika .Matitatizo hayo ndio yalikuwa chachu ya msingi ya wanafalsafa mashuhuri duniani kukaa na kutafakari njia mbadala itakayotatua matatizo hayo ya wafanyakazi.
Hapo ndipo wakina Robert Owen ,Simon Decomte na Charles Fourier walipoanzisha Ujamaa (Socialism). Watu hawa walitafuta neno la Socialism ili kupata wafuasi wengi watakaokuwa na kiu ya kutaka usawa.Hatua hii ya kwanza ilipewa jina la Utopian Socialism (Ujamaa ujenzi)1750s-1850s.
Katika hatua hii ya awali wajamaa wote walijiwekea misingi yao .Misingi hiyo ilikuwa ni kuhubiri ujamaa kwa njia ya amani bila kuleta vurugu .Pia kudai mabadiliko ya kisiasa katika katika ubepari kwenda katika ujamaa kwa njia ya amani.Kuanzishwa kwa mfumo wa Serikali kutoa huduma muhimu kwa raia, kuondoa matabaka kati ya walionacho na wasionacho na kuweka rasilimali zote mikononi mwa raia wote si kwa watu wachache, kubinafsishwa ardhi kubwa na viwanda.
Baada ya hatua hiyo ya wajamaa ujenzi ilifuata hatua nyingine ya kijamaa iliyojulikana kama Scientfic Socialism ujamaa wa kisayansi(1860s-1920s).Ujamaa huo uliongozwa na Carl Marx na Fredrick Engel ambao walikuwa na mtazamo unaofanana.Wao walikuja na vitabu vyao Das Capital na Communist Manifestal vitabu ambavyo vilikuwa vimesheheni nadharia muhimu za ujamaa.Vitabu hivyo vilitapakaa dunia nzima vikitoa mwelekeo wa watu wa tabaka la chini wafanyakazi kupata nafuu kiuchumi kupitia siasa nzito zilizokuwa zimejadiliwa na wanafalsafa hao.
Misingi ifuatayo ndio iliyikuwa imejikita katika hatua hii ya ujamaa .Kuhakikisha chama cha wafanyakazi kinaundwa na kutatua matatizo yao.Kupiga vita unyanyonyaji uliokuwa ukifanywa na mabepari.Kupunguza masaa ya kufanya kazi kwa wafanyakazi wa viwandani kutoka msaa 12 hadi masaa 8.Kuwang’oa mabepari kwa kutumia maandamano na mapinduzi kama njia ya Diplomasia itashindikana.Kuhakikisha kuwa bara la Afrika na Ulimwengu wote watu wote wanakuwa huru chini ya mfumo wa Ujamaa.Kupiga vita kodi za uzalishaji.Pia walitoa changamoto juu ya kutolewa kwa sadaka katika nyumba za ibada ambapo Carl Marx alitoa wito kwa kusema hakuna haja ya kutoa sadaka kwa ajili ya Mungu maana kutoa sadaka ni kudhihirisha kwamba Mungu mnaemwabudu ni dhaifu hawezi kuishi kwa kujitegemea yeye mwenyewe hadi mtoe rushwa aweze kuishi.Pia Carl Marx alishambulia imani za kidini kwa kiasi kikubwa ili kudhoofisha ubepari ambao ulionekana kuwa na uhusiano wa karibu mno na viongozi wa kiimani.
Katika hatua hii ujamaa ulipiga hatua kubwa mno katika kuhakikisha kuwa unatapakaa kila mahali.Hali hiyo ilisaidia kwa mapinduzi ya kijamaa nchini Russia 1719 baada ya Lenin kutumia mbinu za waandishi na wana falsafa mashuhuri katika kuhakikisha anafanikisha mapinduzi .Pia chama cha wafanyakazi kilianzishwa International Labour Organization kikiwa na madhumuni ya kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote duniani wanapata haki za msingi ikiwa ni pamoja na kuboreshewa mishahara yao na hali yao ya utendaji kazi pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na bima na kulipwa pensheni.
Ujamaa ulienea mataifa kama Argentina, China ,Cuba na Afrika .Kutokana na ukweli kuwa wananchi walikuwa wameathirika kwa kiasi kikubwa na mfumo wa ubepari.
Nationalism Socialism (1945s-1990s).Huu ni ujamaa ulianzishwa na kushika hatamu kwa kiasi kikubwa mara baada ya vita vya pili vya dunia 1945s.Nationalism Socialism (Ujamaa wa kuleta uhuru ) Nchi nyingi zilizokuwa zinatawaliwa na mabeberu ziliamua kujiunga na mfumo huo wa ujamaa ili ziweze kupata msaada kwa nchi kama Urusi na Cuba ili wafanikishe azma yao ya uhuru nchi hizo ni kama Kenya ,Ghana na Uganda.Nchi ambazo zilihitaji msaada mkubwa kwa mataifa pingani kwa wakoloni ili wapate msaada wa kujikomboa.Lakini nchi ya Tanganyika kwa wakati ule iliamua kujiunga kwa dhati katika ujamaa kwa kukubali sera na utashi wa ujamaa hususani katika kipindi cha TANU na Mwl Nyerere akiwa kiongozi .
Mwl Nyerere hakusita kubeba dhamana ya ujamaa kwa kuangalia makusudio yake ya msingi na mifumo yote ya aina tatu ya kiuchumi ambayo kila taifa ni lazima liifuate mifumo hiyo ni ;
a) Commanding economy (Uchumi Shurutishi) Huu ni mfumo ambao nchi inaongozwa kwa rasilimali zote za taifa kuwa chini ya Serikali .Na shughuli za huduma za kijamii zinatolewa na Serikali mfano huduma za Afya,elimu, ujenzi wa miundo mbinu .Umoja wa mataifa ,Mashirika na makampuni kumilikiwa na Serikali na kutokuwepo kwa wawekezaji binafsi .Hakuna ushindani wa kibiashara
b) Pure Capitalism Economy (Uchumi wa Kibepari)Mfumo huu umejikita zaidi katika kutoa uhuru kwa wawekezaji kuwekeza katika idara zote za kiuchumi ikiwa pamoja na idara ya Elimu,Afya,na kilimo.Kazi kubwa ya serikali ni kukusanya kodi kwa wawekezaji.Hapa kuna ushindani mkubwa wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa,
c) Mixed Economy (Uchumi Ingiliani) Huu ni mfumo wa kiuchumi anbao umejikita zaidi katika kutaa 50% wawekezaji kuwekeza katika shughuli za kiuchumi na 50% Serikali inamiliki mfumo mzima wa mahitaji ya msingi ya raia na kuwatatulia matatizo.
Mifumo hiyo ya kiuchumi ambayo ni ya aina tatu inakwenda sambamba na aina tatu muhimu za bajeti (budget) ambazo zinashabihiana sana kwa tabia .Nchi yeyote duniani ni lazima iwe na bajeti ya aina hizi.
a) Deficit Budget (Bajeti Pungufu) Katika ukusanyaji wa mapato taifa linakusanya fedha kidogo ukilinganisha na mahitaji yanayotakiwa.Mataifa mengi yenye bajeti ya aina hii urandana sana na mfumo wa commanding economy (Uchumi shurutishi)
b) Standard Budget(Bajeti linganifu) Hii ni aina ya bajeti ambayo makadirio ya fedha ya matumizi na fedha iliyokusanywa vina uhusiano wa karibu sana .Mataifa yenye mfumo huu wa bajeti una randana sana na mfumo wa kiuchumi wa mixed economy (Uchumi Linganishi)
c) Surplus Budget (Bajeti ya ziada)Huu ni mfumo ambao makadirio ya matumizi ya fedha za Serikali ambapo fedha za Serikali zilizokusanywa ni nyingi zaidi kuliko matumizi ya fedha zilizopo.Mfumo huu unajikita zaidi katika mfumo wa uchumi wa Pure Capitalism economy (Uchumi wa kibepari)
Hivyo Mwl Nyerere kwa kuzingatia mifumo hiyo alikuwa na sababu ya kujiunga na ujamaa ili kukidhi mahitaji muhimu ya watanzania.Pia Mwl Nyerere aliona mifano wa mataifa ambayo yalichukua mfumo wa ujamaa na kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa wakati ule.Mataifa kama Russia ,Argentina na Cuba .Mwandishi mashuhuri wa vitabu vya historia na mwanafalsafa I,Chekharin (The state and social system in USSR (Pg 5) anasema “Ujamaa ni mfumo wa kimapinduzi uliopelekea kuondoshwa kwa mfumo wa ubinafsi katika kumiliki rasilimali za umma,pia ndio umekuwa mwisho wa unyonyaji kwa watu wa tabaka la chini pia umoja wa kitaifa umejengwa”
Hali hii ilimpelekea Mwl Nyerere kuunda Azimio la Arusha mwaka 1967 lilikuwa limebeba taswira ya ujamaa.Kwa kuzingatia vya kijamaa Azimio la Arusha liliainisha kwamba binadamu wote ni sawa kwamba kila mtu anastahili heshima bila kujali ana kipato au hana kipato.Kila raia alitambulika kuwa ni sehemu na mahali katika Tanzania pia kila mtu alikuwa na haki ya kupata hifadhi.Katika hatua hii Tanzania ilianzisha vijiji vya ujamaa na kujitegemea lengo na madhumuni ilikuwa ni kuhakikisha kuwa ardhi inatumika kwa maslahi ya watanzania.
Katika kipindi hiki cha Nationalism Socialism (Ujamaa uliojikita katika Uhuru) kazi kubwa kwa nchi zote zilizosadiki ujamaa ilikuwa ni kuhakikisha mataifa yote ya Afrika yanapata Uhuru.Tanzania ikiwa ni nchi mwanachama.Zama hizo zilianza 1945s-1990s kipindi hiki kilikuwa cha ujamaa uliojikita katika kuleta uhuru barani Afrika.
Zama za Modern Socialism (Ujamaa wa kisasa ) 1990s-2015s Hiki ni kipindi cha ujamaa uliopevuka au ujamaa wa kisasa ambao umeboresha maeneo yote ambayo yalionekana kuwa pingamizi katika kuleta maendeleo mfano ni kuondoshwa kwa vijiji vya ujamaa na kujitegemea ambavyo havina tija kwa sasa lakini mizizi ya misingi ya ujamaa bado inaonekana ikiwa ni pamoja na kuwa na mfumo wa Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake moja kwa moja pia bado watu wanashirikiana kwenye misiba na sherehe hata kama hawajaalikwa.Serikali inatoa huduma zote muhimu katika nyanja zote muhimu mfano ni Idara ya elimu na afya kwa kuwa na shule za Serikali na Hospitali za Serikali..Mala baada ya kuangalia mifumo na hatua muhimu za ujamaa ni vyema pia kuutazama mfumo wa kibepari ili tuweze kujadili kwa kina Tanzania itakuwa katika mfumo upi wa kati ya ujamaa au ubepari?.pia ni vyema kujua ubepari ni nini.
Ubepari umetokana na neno Capitalism ambalo mzizi wake ni neno Capital (mtaji) na mfumo huo umeanza kushika hatamu Ulaya tangu karne ya 15th C Mfumo huu ulijikita zaidi kwenye biashara .Pia muundo wake wa kijamii na kisiasa umejikita katika ubaguzi wa hali ya juu kati ya waliokuwa nacho ambao ndio wenye maamuzi katika nchi,na wasiokuwa nacho ambao kazi yao ni kutekeleza majukumu kutoka kwa walionacho.Katika nchi zinazoendeshwa kwa mfumo wa kibepari,mabepari wanalipa kodi kwa kiasi kikubwa hali inayopelekea Serikali kuwa na fedha za kutosha kuliko mahitaji (surplus budget).Katika nfumo wa kjbepari hakuna mwingiliano wa kijamii kila mtu ataishi kwa uwezo wake mwenyewe .Uwekezaji kwa watu binafsi katika nchi ni asilmia 100% Serikali ni kukusanya kodi tu.Ubepari umejikita katika utabaka kwa dhati mwanafalsafa wa kibepari Rugner Nurks anatoa falsafa iliyoungwa mkono sana na mataifa ya kibepari inayosema “Mtu tajiri ni lazima apewe elimu ya utajiri ili aulinde utajiri wake na mtu maskini apewe elimu ya umaskini ili ajue vema umaskini wake” na huo ndio utofauti mkubwa kati ya ubepari na ujamaa.