Na Sakina Sahabani wa Xdeejayz Tanzania
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua Msanii Manaiki Sanga a.k.a The Don ameibuka na kumuumbua vibaya msanii mwenzake Diana Kimario ambae siku za hivi karibuni amekuwa akijitangaza kama yeye ni bkra yani hajawahi kuguswa na mwanaume kwa kushiriki tendo la ndoa.
Jambo hilo limepingwa vikali na Manaiki ambae anadai ameishi na Diana kama mkewe zaidi ya mwaka na nusu huku Mamaake Diana anaeishi Manzese akiwa shahidi namba mjoa.
Diana mara kadhaa amekuwa akijitangaza kama yeye hajawahi kuguswa na mwanaume na wala hajui chochote kinachoitwa ngono kwani tangu azaliwe hajawahi kushiriki tendo hilo la kikubwa.
Aidha mtandao huu ulimtafuta Diana ili kujibu hoja ya Manaiki Sanga lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana hadi habari hii inaruka hewani na kuwafikia wasomaji wetu makini.
SOURCE: XDEEJAYZ TANZANIA